Ulanguzi Tiketi za Mayweather na Manny Pacquiao Waanza, Sasa ni Sh. Milioni 240 Kwa Tiketi Moja Badala ya Sh. Milioni 130,000


Wajanja wa mjini waliobahatika kununua tiketi za awali za mpambano wa masumbwi unaosubiriwa kwa hamu kubwa duniani kote kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao, wameanza kutumia nafasi hiyo kwa kuwauzia wengine ambao walichelewa kufanya manunu ya tiketi hizo.

Tiketi za mpambano huo zilianza kuuzwa majira ya jana jioni kwa saa za mjini Las Vegas nchini Marekani na iliwachukua wajanja hao kuzinunua kwa dakika chache.

Tiketi moja ilitangazwa kuuzwa kwa dola za Kimarekani 70,790 (sawa na Sh. Milioni 130,000), lakini baada ya dakika chache tu ziliisha katika mitandaoni.

Nafasi hiyo iliwapa fursa wajanja hao kuanza kuziuza tiketi walizo zinunua kwa dola 128,705 (Sh. Milioni 240) kwa tiketi moja.
Baada ya majuma kadhaa yaliyochukua nafasi kwa washindani wawili wa mpambano huo wa May 2 mwaka huu, kiasi cha tiketi 500 na 1,000 ziliingizwa sokoni jana kwa ajili ya pambano la utajiri mkubwa.

Mashabiki waliokua wamejiandaa kuushuhudia mpambano huo wakiwa ukumbini, walikuwa tayari kununua tiketi za ‘bei poa’ kupitia mgmgrand.com na ticketmaster.com.

Tiketi za bei ya chini ambazo zilitangazwa mwanzo gharama zake ni kuanzia dola 1,500 (Sh. Milioni 2.7), lakini na huko zimepanda hadi dola 7,500 (Sh. Milioni 13.8) kwa siti.

Wajanja (Walanguzi) wa awali walidhibitiwa kutonunua zaidi ya tiketi nne kwa mtu mmoja.
Hata hivyo tiketi za dola 10,000 (Sh. Milioni 18.5) hazikuingizwa sokoni na zinatarajiwa kupanda hadi dola 200,000 (karibu Sh. Milioni 400).