Mambo matatu aliyoyasema Jerry Murro kuhusu sakata la mchezaji wa Simba Ibrahim Ajibu


Jerry Muro: “Mchezaji Ibrahim Ajibu tumebaini ana kadi nne za njano alizoonyeshwa katika mechi dhidi ya Stand United FC Uwanja wa Taifa Oktoba 4, Polisi Moro FC dhidi ya Simba SC Uwanja wa Jamhuri, Morogoro Februari 15, Stand United FC dhidi ya Simba SC Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga Februari 22 na Simba SC dhidi ya Prisons FC Uwanja wa Taifa Februari 28,” Muro amesema.

“Kutokana na tukio lenyewe kuwa la kidhalimu na lenye kutaka kurudisha nyuma maendeleo ya soka la Tanzania, sisi (Yanga SC) tunaitaka TFF kuingilia kati utata huu kwa kuipoka pointi 3 klabu ya Simba SC ilizozipata katika mechi namba 125 dhidi ya Prisons FC kwa sababu ilitumia mchezaji asiye sahihi katika mchezo usio sahihi kwa mchezaji husika.
“Pili, tunalitaka shirikisho litoe adhabu kali kwa viongozi wote wa Simba SC na mchezaji husika kwa kikiuka kanuni na taratibu za uendeshaji wa ligi.

“Tatu, tunamtaka Kaimu Ofisa Mtendaji wa TPLB, Fatma Abdallah Shibo, ajiuzulu kutokana na kupindisha sheria na taratibu na pia kupotosha umma wa Watanzania kuhusu sheria na kutoa kibali hewa cha kuruhusu mchezaji Ibrahim Ajibu kucheza dhidi ya Prisons huku akiwa na kadi nne za njano,” amesema zaidi Muro.
Chanzo,Shaffih Dauda.