Valentine Yamkalia Ommy Dimpoz Vibaya Azuiliwa Kuingia Marekani Kufanya Show..Arudia Uwanjani

Nasikia viza aliyokuwa amekata haikuwa ina mruhusu kufanya show nchini marekani! Inasemekana alitakiwa kukata viza ambayo inaonesha ana kwenda kufanya show nchini marekani na bila shaka gharama zake ni tofauti na ile ya kwenda kutembea!Viza aliyo kuwa amekata ilikuwa ya kwenda kutembea tuu na kusalimu ndugu na jamaa si kufanya show....


Sasa kilicho tokea alipo fika uwanja wa ndege akazuiwa kuingia nchini marekani kwani viza aliyo kuwa amekata ilikuwa haimruhusu kufanya show ni baada ya kuhojiwa!

Ninacho jiuliza kwanini watanzania tunafikiri kila sehemu tunaweza kufanya ujanja ujanja? Kwanini hatupendi kufata utaratibu?Bahati mbaya zaidi show ilikuwa imesha andaliwa na jana kama si juzi ilibidi afanye!

Yani mtu anataka pesa halafu anaogopa kuingia gharama kukata viza itakayo mruhusu kufanya show nchi ya watu!