Yanga yagomea ushindi wa Simba FIFA

Yanga jana wameliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga ushindi wa Simba walioupata dhidi yao Jumapili iliyopita wakitaka wanyang’anywe pointi tatu na kama TFF itashindwa kufanya hivyo basi wameweka wazi dhamira yao ya kulipeleka suala hilo mpaka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kutafuta haki yao.

Kikubwa kilichoifanya Yanga kufikia uamuzi huo na kuitaka Simba ipokonywe pointi hizo ni baada ya Simba kumchezesha mchezaji wao, Ibrahim Ajibu mwenye kadi tatu za njano.

Awali kabla ya mchezo huo, Yanga ilituma barua TFF kutaka kujua ni kanuni ipi inamruhusu mchezaji mwenye kadi tatu kuchagua mechi za kucheza wakati ipo wazi kwamba anapaswa kukosa mechi zinazofuata kisha akaendelea na nyingine, lakini ilikosa majibu na ndipo ikaamua kuandika nyingine iliyotumwa jana iliyojumuisha na azimio jingine la Simba kunyang’anywa pointi tatu.


Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, alifafanua kuwa endapo kama wao wangeshinda mchezo huo basi ingebidi Simba wapigwe faini lakini kwa kuwa wameshindwa, basi inapaswa Simba wanyang’anywe pointi tatu ambapo alisisitiza kuwa katika hilo hawatarudi nyuma mpaka wapate haki yao stahiki.

“Tumeandika barua leo (jana) mapema na tayari tumeshaipeleka TFF kuhusu kutaka Simba kupokwa pointi walizozipata kwenye mchezo wetu wa Jumapili kwa kuwa walimchezesha Ibrahim Ajibu, mwenye kadi tatu za njano, kitu ambacho ni kinyume na kanuni za soka zinavyotaka.

“Na kama itatokea TFF watakosa jibu stahiki la kutupa au kushindwa ‘ku-solve’ kesi hii, basi sisi tutasonga mbele na tutakwenda Caf (Shirikisho la Soka Afrika) na kama hapo pia itakosa ufumbuzi basi tutafika mpaka Fifa, ilimradi tuhakikishe haki yetu inapatikana.

“Kama ingekuwa tumeshinda sisi siku ile, basi Simba lazima ingepigwa faini lakini kwa kuwa wao wameshinda basi adhabu yao ni kupokonywa pointi tatu, hata mechi zao walizocheza na Stand United na Prisons pia zinapaswa kupokonywa pointi kwa kuwa walikiuka kanuni kama hii.

“Kitu cha kujiuliza ni kwamba kanuni zinawezaje kubadilishwa bila ya wahusika ambao ni timu za ligi, kuwa na taarifa isipokuwa Simba pekee