Unahisi Adhabu Gani Inawafaa Waganga ama Watu Wanaohusika na Mauaji ya Albino?

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limewakamata waganga wa kienyeji 55 wakiwa na viungo vya binadamu vikiwemo meno na nywele vinavyodaiwa kuwa ni vya watu wenye albino. Inasemekana waganga ngio huagiza watu viungo vya albino ili wawafanyie dawa.

Kwa maoni yako, watu hawa wanaosababisha ndugu zetu albino wanauwawa, unahisi adhabu gani inawafaa?