Mashabiki watakiwa kutowapa lawama magoli kipa

Viongozi wa Vilabu na mashabiki nchini wametakiwa kuachana na tabia za kutoa lawama kwa magoli kipa wanaofungwa magoli mbalimbali ikiwemo kuhama goli na hatimaye kuweza kufungwa.

Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa Kituo cha Magoli Kipa nchini TGC, Peter Manyika amesema, katika mazoezi kipa anafundishwa na kutahadharishwa mambo mbalimbali hususani kulinda goli inapotekea hatari ya kufungwa.
Manyika amesema, mashabiki na viongozi wanapoendelea na lawama watakuwa wanabadilisha magolikipa kila kukicha kwani kila Golikipa anakuja na tatizo lake na suala linalotakiwa ni kufundishwa zaidi ili kuweza kufanya vizuri na wapo magoli kipa wanaofundishwa lakini wanafungwa aina ya magoli ambayo huzuilika.
Manyika amesema, Golikipa anakuwa amebeba jukumu la watu wote hivyo suala la kufanya makusudi ili aweze kufungwa katika mechi mbalimbali linakuwa ni gumu kwania anaamini kila mtu anamtegemea yeye awapo langoni.
--------------
Note: