Mzee Malecela amekitaka Chama cha Mapinduzi Kumchukulia hatua kali za kinidhamu Lowassa


Maneno aliyosema mwl. Nyerere kuwa IKULU sio pango la walanguzi usikimbilie kwenda IKULU ni mahali patakatifu mtu yeyote anayekimbilia IKULU bila kujiuliza mwogopeni hafai kuwa Rais. Maneno hayo ya mtu kukimbilia IKULU aliyarudia kuyasema Waziri mkuu mstafu mzee John Malecela.

Mzee john malecela amekitaka chama cha mapinduzi CCM kumchukulia hatua kali waziri wa zamani aliyefukuzwa na bunge la Tz Edward Lowassa kwa kitendo cha kugawa fedha nchi nzima kugawa Boda boda nchi nzima kugawa Tisheti nchi nzima zilizoandikwa kwa jina lake Lowassa.

Mzee malecela amesema mtu huyo hafai kuwa kiongozi hafai kuwa hata Balozi wa nyumba 10 anagawa fedha ili awe Rais ananunua urais kwa fedha pesa hizo atazirudisha kwa njia gani? Kwa nini asipumzike kama nilivyopumzika mimi na maswala ya urais mtu huyo hafai.

Mzee malecela amesema wapo baadhi ya wapambe wake wamekuwa wakisema Lowassa anataka urais ili atimize ndoto zake hata akipewa wiki mbili zinatosha kutimiza alichotamani kwa muda mrefu jiulizeni hapo kuna kitu gani nyuma ya pazia kilichojifich Pia mzee malecela amesema sizungumziii wizi wa Lowassa tuhuma zake maana kila mtu anajua Lowassa jinsi alivyo.

Mzee malecela amesema nawashangaa sana baadhi ya watu wanasema Lowassa mchapa kazi ana maamzi magumu sio kweli mimi namfahamu vzr sana Lowassa nilifanya naye kazi ofisini kwangu nikiwa waziri mkuu lkn nilishangaa sana kusikia Lowassa ameteuliwa kuwa waziri mkuu nilisema kijana huyo hatadumu kwa muda mrefu kwenye hiyo nafasi.

Mzee malecela amesema Watanzania waliona Lowassa alipokuwa waziri mkuu alianzisha njia tatu mkoa wa dar es Salaam ili kupunguza foleni bila kufuata sheria zilizowekwa watu wengi sana walikufu na wengine wameshakuwa vilewa wa miguu pia aliagiza jengo la golofa 10 lilipo masaki karibu na nyumbani kwake livunjwe.

Jengo hilo lilifunjwa na suma JKT. bila kufuata sheria matokeo yake serikali ilishindwa na kuamliwa na mahakama kumlipa mwenye Jengo hilo mamilioni ya pesa serikali ililipa hela za umma na aliyesababisha upotevu wa fedha za umma ameachwa yupo anadunda mitaani mambo mengi yalitokea kipindi akiwa waziri mkuu leo hii ndio awe mwenye maamzi magumu.

Mungu anamjua Rais aajaye chama kinamjua atakaye kuwa Rais pia serikali inajua urais wa nchi hautafutwi kwa namna hiyo ameongea mzee John Malecela waziri mkuu mstafu wa Tanzania.