H-Baba asema lazima mwanaye aishi kisanii kama wazazi wake,afunguka kuhusu kumuweka 'bleach'
Msanii wa bongo Fleva,H: Baba amewafungukia mashabiki wake waliomjia juu
baada ya kumuweka dawa ya nywele'bleach' mtoto wake,Tanzanite mwenye
umri wa mwaka mmoja.
Mashabiki walimwambia msanii huyo kuwa bleach siyo nzuri kiafya kwa
mtoto huyo,H: Baba akijibu tuhuma hizo alisema kuwa lazima mwanaye aishi
kisanii kama wazazi wake na kwamba yeye kama mzazi hawezi kumuharibu
mtoto wake.
'Watu wanashindwa kuelewa mimi sijampaka mwanangu bleach hiyo ni hina
pia hina ni suna kwa dini yetu ya Kiislam sioni tatizo hapo,'alisema H:
Baba.