Diamond, Ommy Dimpoz, January na wengine walaani mauaji ya albino

Mauaji ya mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja, Yohana Bahati huko Chato yamewaumiza watu wengi si Tanzania tu bali dunia nzima.

Kifo cha kusikitisha cha mtoto huyo aliyekutwa amekatwa miguu na mikono kimeandikwa na mashirika yote makubwa ya habari duniani na hivyo kuipa Tanzania sifa mbaya.

Wananchi wamelaani vikali kitendo hicho na kuitaka serikali kuchukua hatua kuhakikisha haviendelei tena. Hivi ndivyo mastaa wa Tanzania nao walivyoungana na wananchi wengine kueleza waliyonayo moyoni.

Diamond

Ndugu zangu! nafkiri ni Muda wa kubadilika sasa…Tuacheni fikra potofu, za Kipuuzi na ukatili Usio na Maana.. Hivi inamaa unataka kuniambia na hao kina Bill gates Mzee wa kuku, Carlos Slim, Amancio Ortega , Bakhresa na Matajiri wakubwa Duniani pia Walitajirika kupitia Ukatilii huu wa Ma Albino…??? Juhudi na Utendaji wako wa Kazi ndio utao kufanya Uendelee na kufikia Hayo Malengo unayoyataka… Tuache kujidanganya na Kuwatesa Ndugu zetu wasio na Hatia.

Ommy Dimpoz

Tanzania inazidi kupata sifa mbaya kimataifa kila kukicha. Ufisadi, rushwa na sasa mauaji ya albino wasiokuwa na hatia yamerudi tena. Inasikitisha kuona kwamba kuna binadamu yupo radhi kumuua binadamu mwenzake ili apate utajiri. Hii haikubaliki hata kidogo.

Naungana na watanzania wote walioumizwa na mauaji ya mtoto Yohana Bahati wa huko Chato kulaani vikali kitendo hicho. Serikali ichukue hatua madhubuti kulinda usalama wa ndugu zetu hawa. ‪#‎PingaUkatiliHuu‬ ‪#‎StopAlbinoKillings‬

Lady Jaydee

Sio vizuri Sio vizuri kabisaaa Nadhani sote tunafahamu fika Kuwa sio vizuuuuuri Ila kwanini tunaendelea kufanya Wakati tunajua sio vizuri Tafadhali Angekuwa mwanao? Angekuwa kaka /dada yako? Angekuwa mdogo wako? Ungejiskiaje? Kumbuka tu kuwa, sio vizuri. Full stop.

Zahir Zorro

Tazama Watoto hawa walivyo wazuri, Sera ya kujua Albino inaleta LAANA. Kubwa sana ktk Tanzania. Hivi Tujiulize anae faidika ni nani??

Peter Msechu

#Nihakiyakekuishi HUYU NI BINADAMU KAMA WEWE MWENYE MAUMIVU KAMA WEWE MWENYE MOYO WA NYAMA KAMA WEWE INAUMA SANA KUONA BAADHI YA WAPUMBAVU WACHACHE WANAMGEUZA BINADAMU MWENZAO BIASHARA KWA KUTOA UHAI WAKE HII NI DHAMBI KUBWA SANA SANA MUNGU ANACHUKIZWA SANA NA KITENDO HIKI KINAVYOENDELEA HAPA TANZANIA.. TUNAJITIA LAANA WENYEWE BILA KUJUA TUTASHINDWA KUFANIKIWA NA TAIFA KUZOROTA SABABU YA ROHO HIZI ZINAPOANGAMIA BILA SABABU WATANZANIA WENZANGU TUUNGANE KWA PAMOJA TUKEMEEE MAUAJI HAYA #TEAM #TUPENDANEEE

January Makamba

Mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi, yaani albino, ni ukatili usio na mfano. Serikali haipaswi kuwa na huruma katika kuwasaka na kuwaadhibu wanaofanya vitendo hivi. Ni muhimu pia kuweka utaratibu wa kuwalinda wenye ulemavu wa ngozi dhidi ya tishio la kutekwa na kuuwawa. Elimu kwa umma ni muhimu. Wanaofanya haya matendo wapo ndani ya jamii yetu. Tuweke utaratibu wa malipo kwa wasamaria wema wanaotoa habari kuhusu wahusika wa biashara ya viungo vya binadamu. Na tuweke utaratibu wa kuwalinda watoa habari hizi. Hili ni tatizo la kisheria lakini pia ni tatizo la imani za ushirikina na uchawi ndani ya jamii. Ni lazima kuyakabili mambo haya mawili kwa pamoja. #TanzaniaMpya @TanzaniaMpya #StopAlbinoKillings

Henry Mdimu

Ni kweli mimi ni Albino, nimejikubali na nimeishi maisha yangu yote bila kujali nilivyo. Sijawahi kutumia hali yangu kupata kitu kwa huruma, nimeyapigania maisha yangu na nimepiga hatua. Leo hii naongea nanyi nikiwa Baba, Mume, Mwandishi Mwandamizi, Blogger, na mengine mengi, lakini hali yangu sasa inaanza kunikwaza. Haya mauaji jamani, nimejiteua kuwa Balozi, nitatetea, na kusimama mbele ya wenzangu wote wenye hali kama hii, kama ni wanasiasa ama wafanyabiashara, wanataka kutuua kwa maslahi binafsi, mwaka huu HAPANA. Wanaoniunga mkono mikono juu